MATOKEO DARASA LA SABA ZANZIBAR 2024/2025
Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa rasmi leo Zanzibar. Katika makala hii fupi utaweza kutazama matokeo ya darasa la saba waliofanya mtihani wa upimaji mwaka 2024 na kuona ufaulu wa kila shule zilizopo Zanzibar. Kupitia tangazo hili la matokeo mzazi ataweza kujipanga na kufanya maandalizi kwa mtoto wake kwa kumnunulia mahitaji ya shule baada ya kupata fomu ya kujiunga elimu ya kidato cha kwanza 2025.
Matokeo ya Mtihani huu yametoka mwishoni mwa mwaka 2024 ambapo wazazi pamoja na walezi wapo busy na maandalizi ya kupokea mwaka mpya hivyo inaleta mshituko kwa walezi na kuweka akilini kuwa baada ya sherehe za kuuaga mwaka basi ni maandalizi ya vijana wao waliopangiwa kujiunga kidato cha kwanza 2025.
Tanzania bara ilitangaza matokeo mapema kabla na tayari fomu za kujiunga kidato cha kwanza zimeshaanza kutolewa kwa kila shule katika mikoa yote hivyo wazazi na walezi wanafanya maandalizi kulingana na kilichoelezwa kwenye fomu hizo.
MATOKEO DARASA LA SABA ZANZIBAR
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MAANDALIZI YA MWANAFUNZI KABLA YA KURIPOTI SHULENI
1. Hakikisha anapata vipimo vyote vya afya kama fomu ya kujiunga inavyoeleza
2. Nenda hospital za serikali na hakikisha mtoto anapimwa na kupewa risiti.
3. Mwanafunzi ashonewe sare za shule husika kama utakuwa na wasiwasi nenda shule kuchukua smple kama kitakuwepo.
4. Mwanafunzi aripoti shule mapema na asichelewe.