Form Five Selection and College 2025 - Uchaguzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025
Karibu Shuleforum, katika makala hii tutakuletea Kiunganishi cha kutazama Form Five Selection and College 2025 - Uchaguzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025. Form Five Selection ni hatua inayofuata baada ya kutangazwa matokeo ya mtihani wa upimaji kidato cha nne 2024, kwa wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na masomo ya kidato cha tano watapangiwa shule kulingana na masomo waliyofaulu na kuyachagua (combination) pamoja na wale waliochagua kujiunga na vyuo vya kati watachaguliwa na kupangiwa vyuo hivyo kulingana na ufaulu wao.
Nini unaweza Kufanya Kwa Sasa Wakati unasubiri kutangazwa kwa Selection za Form Five na Vyuo vya Kati - Uchaguzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025
Kwasasa ni muhimu zaidi kujiandaa kifedha kwani baada ya kutangazwa kwa uchaguzi kidato cha tano kutakuwa na muda mchache sana wakuripoti shuleni, utakapojiandaa mapema kwa msaada wa wazazi itakuwa ni vizuri zaidi kwani unaweza kuchaguliwa mkoa wowote hapa Tanzania.
Jinsi ya Kuangalia Selection Form Five - Uchaguzi kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025
Shuleforum itakuletea link yenye majina ya wanafunzi waliochagua kujiunga na vyuo vya kati pamoja na kidato cha tano 2025/2026 kupitia makala hii baada ya selection hizo kutangazwa mwezi huu wa sita.
Unachotakiwa kufanya wewe kama mwanafunzi au mzazi unayesubiria Chaguzi za Kujiunga kidato cha tano na Vyuo vya kati ni kujiunga na magroup yetu ya whatsapp na Telegram ili uweze kupata updates haraka baada ya kutangazwa kwa Form Five Selection June 2025.
BONYEZA HAPA KUANGALIA SELECTION FORM FIVE 2025
Je Mwanafunzi anaweza kuchaguliwa Mkoa wa Mbali na mahali aliposomea Ordinary Level?
Inawezekana Kabisa, Mwanafunzi anaweza chaguliwa kujiunga kidato cha tano shule yoyote nchini Tanzania. Mfano alimaliza kidato cha nne mkoa wa KIGOMA anaweza kupelekwa shule za Tanga, Kilimanjaro au Morogoro au hata Kuchaguliwa Shule za hapohapo Kigoma.
Je Joining Instructions zinapatikana Wapi?
Baada ya Kutangazwa kwa Uchaguzi Kidato cha tano na vyuo vya kati 2025 kupitia website ya Tamisemi mwanafunzi ataweza Kudownload joining instruction Pdf yake kwa kugusa jina la shule alipopangiwa Kwenda kujiunga na masomo ya kidato cha tano 2025.