Kiswahili Notes Kidato cha Pili - Kiswahili Notes Form Two
MADA YA KWANZA: UUNDAJI WA MANENO
Uundaji wa
maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa
maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano.
Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na
kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano
tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na
mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
Kutumia Uambishaji
Kubainisha Mofimu katika Maneno
Uambishaji wa maneno ni kitendo cha
kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea
kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda
maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazobadilika kwenye kiini
cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili viambishi
hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano
Wanapendana = Wa-na-pendan-a
kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu
zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini
cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya
kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Example 1
Angalia mifano ifuatayo:
Neno |
Viambisha
Awali |
Kiini
Viambisha |
Tamati |
Unapendelea |
u-na- |
-penda |
el-e-a |
Waliongozana |
wa-li- |
-ongoz- |
an-a |
Analima |
a-na- |
-lim- |
-a |
Anayeiimbisha |
a-na-ye |
-imb- |
-ish-a |
Dhima za Mofimu
Bainisha dhima za mofimu
Baadhi ya dhima za uambishaji ni
kama ifuatavyo:
- Kuonyesha upatanisho wa usanifu
maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu,
lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha
kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia
mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji,
fundishwa, fundishana.
- Uambishaji huonyesha nafsi
- Uambashaji huonyesha njeo
(muda)
- Uambishaji huonyesha urejeshi
- Uambishaji huonyesha ukanushi
- Uambishaji huonyesha hali
mbalimbali za kitenzi
Vitenzi
vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.
Mfano.
2
Mfano
Vitenzi |
Kiini |
Nomino |
Vitenzi |
Cheza |
-chez- |
Mchezaji, mchezo |
wanacheza/atamchezea |
Piga |
-pig- |
Mpigaji, Mpiganaji |
watanipiga,
aliyempiga/wanaompiga |
Uambishaji
hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.
Neno
(Kiwakilishi) |
Kiini |
Kielezi |
Huyu,
Huyo |
Hu |
Humu,
humo |
Wangu,
wako,wake |
Wa |
|
Hii,
hizo, hiki |
Hi |
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza
nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano: Hawakulima
- Ha-, kiambishi cha ukanushi
- Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi tamati vina dhima
mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na
kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na
mtendwa, ukamilisho, usababishi.
Mfano 3
Neno |
Viambishi
Tamati |
Anapiga |
-a |
Wanapigana |
-an |
Asipigwe |
-w |
Amempigisha |
-ish- |
Viambishi tamati vina dhima ya
kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.
Neno |
Kiini |
Viambishi
Tamati |
Piga |
pig- |
-o |
Mchezo |
chez- |
-o |
Mtembezi |
tembe- |
-z-i |
Mfiwa |
-fi- |
-us-a |
Kutumia Mnyumbuliko
Mazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno Mapya
Elezea mazingira yanayosababisha
mahitaji ya maneno mapya
Mnyumbulisho ni neno linalotokana na
neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.
Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili
ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo
basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya
kunyumbulisha.
Viambishi vinapochukuliwa katika
kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini
chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa,
lim-ia, lim-w-a.
Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza
kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa mfano:
Neno |
Kiini |
Shina |
Maneno
ya Mnyumbuliko |
Elekea |
elek |
Eleka |
Elekeana,
elekea, elekwa, elekesha |
Shikishana |
shik |
Shikisha |
Shikishana,
shikisha, shikishaneni |
Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa
maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza
kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi mmoja wa maana.
Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa Maneno
Dhima ya uambishaji ni kuleta
upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika ngeli za
majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa
uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni
kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi
baada ya mzizi wa neno.
Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia
Mnyambuliko
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia
mnyambuliko
Uundaji wa maneno mbalimbali kwa
kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na
hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo
pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.
Zoezi 1
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia
mnyambuliko
Kutumia Maneno ya Mnyambuliko katika
Miktadha mablimbali
Tumia maneno ya mnyambuliko katika
miktadha mablimbali
Maneno ya mnyambuliko hutumika
katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli
mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli
ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli
ya kutendana, na kauli ya kutendama.
Zoezi 2
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbali.
MADA YA PILI: MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIKTADHA MBALI
MBALI
Matumizi ya lugha ni namna ambavyo
wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa kuzingatia mila, desturi na kaida
mbalimbali za jamii inayohusika.
Rejesta
Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta
kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na
uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande
mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha
fasaha, mfano katika elimu, mahakamani na kadhalika.
Kuwasiliana kwa kutumia Rejesta
Rejesta za Mitaani
Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa
magengeni nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka
kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Mfano wa maneno yanayotumika
sana mitaani ni kama vile “Mshikaji” (rafiki) Demu” (mwanamke)n.k. Kwa ujumla
lugha ya mitaani ni lugha isiyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mitaani
ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe.
Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali)
Mazungumzo ya kwenye shughuli
maalumu hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum
zinazojitokeza katika mazingira haya. Kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu
kwenye mazingira yale yale.
Mazungumzo ya kwenye shughuli
maalumu ni kama vile mazungumzo ya:
- Maofisini
au mahali popote pa kazi
- Mahakamani
- Hotelini
- Hospitalini
- Msikitini
- Kanisani n.k
Mazungumzo ya mahotelini yana
utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida inaweza isieleweke.
Nani wali kuku?
B: Mimi
Chai moja wapi?
B: Hapa
Katika mazungumzo haya A anapouliza
“Nani wali kuku”, ana maana kuwa nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku”.
Hapa hana maana ya kumwainisha mtu aitwaaye “wali kuku”.
Kwa upande wa lugha ya mahakamani ni
tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya mahakamani inasisitiza usahihi ili
kuondoa migongano miongoni mwa wanaohusika.
Mfano 1
Mfano:
Wakili wa Utetezi: Nakuuliza jaribio
la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la namna gani katika sheria za
Tanzania?
Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa
kitabu cha sheria za Tanzania na kukisoma) Ni kosa la uhaini.
Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda
mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili hawahusiani na makosa haya?
Kamishna Msaidizi: Sijui.
Kimsingi hii ni hali ya kawaida
kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara nyingi mahojiano katika mahakama
hayaendi haraka sana. Kila mtu anayehusika – hakimu, mwendesha mashtaka,
wakili, mdaiwa, shahidi, n.k. hujieleza kwa wazi wazi bila kujali urefu wa
maelezo.
Rejesta Zinazohusu Watu
Rejesta zinazohusu watu ni yale
mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku au
mazungumzo rasmi; kwa mfano mazungumzo kati ya:
- Vijana wenye rika moja,
- Wazee wenyewe,
- Wanawake wenyewe,
- Wanaume wenyewe,
- Mwalimu na mwanafunzi,
- Meneja na wafanyakazi wake,
- Mtu na mpenzi wake, n.k.
Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa
rika moja huzungumza lugha ambayo wao wenyewe wanaielewa na sio rahisi kwa mtu
wa rika lingine kuielewa lugha hiyo.
Mfano 2
Mfano:
'Basi, Master jana wikiendi ilikuwa
kibaridi sana. Basi nilizamia infoo kwenye zinga la mnuso huko saiti za
upanga.Nilifika getini nikakuta baunsa kanyuti chedro likisubiri kumtoa noma
kila mzamiaji.Alikuwa mnoko kishenzi. Akatema mkwara mbuzi, nikajibu kwa
mkwaradume....akabloo mimi ndani’.
Maana ya Maneno
- Wikiendi – Mwisho wa wiki
- Kibaridi –tulivu
- Kuzamia infoo – Kuingia mahali
bila kualikwa
- Zinga la Mnuso –sherehe kubwa
- Saiti –sehemu
- Baunsa limenyuti chedro – Ni
mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni
- Noma – Hatari
- Mnoko kishenzi – kinaa sana
- Mkwara mbuzi – Vitisho dhaifu
(Sani, Toleo Na 49).
Mtu asomapo maelezo hayo, mara moja
unaona jinsi vijana hawa wa rika moja waishio mjini wanavyozungumza Kiswahili.
Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuielewa kirahisi lugha hiyo.
Dhima za Rejesta
Katika kipengele cha utambulisho wa
kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha
miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii
husika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika
katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na
jinsi ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika
mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na
mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na
lugha anayotumia.
Rejesta, ina nafasi kubwa sana
katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni
kutokana na kwamba, madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia
wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango
cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa
kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au
vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza
na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.
Pia rejesta inasaidia sana
kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya
kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini
“mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo
mengine.
Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza
idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa
urahisi mfano rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja:
hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa.
Pia katika kutolea elimu ya dini
kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili.
Vilevile rejesta ina nafasi ya
kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda
kutumia maneno tofautitofauti ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Mfano
mazungumzo miongoni mwa vijana:
Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili
Kijana 2: mzuka jembe. Kama kawa… kama
dawa!
MISIMU
Kuwasiliana kwa Kutumia Misimu
Misimu ni semi za muda na mahali
maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. misimu inayodumu
huweza kuingia katika methali, nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo.
Chanzo cha misimu
- Misimu huzuka kulingana na
mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii husika katika nyakati
mbalimbali.
Misimu huzuka kutokana na haja ya watu kuelezea hisia zoa juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea katika vipindi fulani kwa mfano, njaa, mafuriko, vita n.k
Aina za misimu
- Misimu ya pekee. Hii ni misimu ambayo huelezea mahusiano ya kikundi
kimoja kutoka katika utamaduni mmoja, na hujulikana miongoni mwao pekee.
- Misimu ya kitarafa. Misimu hii hujulikana na watu wengi katikia eneo
kubwa, yaweza kuwa ni kata, wilaya au tarafa.
- Misimu zagao. Ni misimu iliyoenea nchi nzima au pengine kuvuka
mipaka ya nchi, misimu hii husikika redioni, magazetini na hata kwenye
vitabu. Msimu uliokita mizizi sana huweza kusanifishwa na kuwa msamiati
rasmi.
Sifa za misimu
- Huzuka na kutoweka kufuatana
na mabadiliko ya jamii
- Ni lugha isiyo sanifu
- Ina chuki
- Ni lugha ya mafumbo
- Ina maana nyingi
Dhima ya misimu
- Hutumika kupamba lugha
- Hutumika kukuza lugha
- Hutumika kutunza historia ya
jamii fulani
- Hutumika kuibua hisia
mbalimbali za wazungumzaji
- Hufurahisha na kuchekesha
Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi
Sifa ya Lugha ya Kimazungumzo
Lugha ya mazugumzo ni maongezi ya
watu wawili au zaidi bila kutumia maandishi. Lugha ya mazungumzo ambayo ndiyo
lugha kongwe zaidi ya lugha ya maandishi ina dhima kubwa ya kufanikisha
mawasiliano miongoni mwa watu au kikundi fulani. Lugha hii ya mazungumzo
ilianza punde tu binadamu alipoanza kukabiliana na mazingira yake, hivyo
kimsingi lugha ya mazungumzo ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha shughuli zote za
kibinadamu kutokana na nafasi yake kimatumizi.
Faida ya lugha ya mazungumzo
- Mzungumzaji anaweza kukaa ana
kwa ana na msikilizaji, hivyo hukuza uhusiano.
- Mzungumzaji anaweza kutumia
ishara za mwili katika kusisitiza maelezo yake.
- Mzungumzaji anaweza kupata
nafasi ya kuuliza au kuulizwa maswali.
- Mzungumzaji anaweza kuonesha
hisia zake kwa kulia, kupaza sauti, kupunguza sauti, kuonyesha furaha
huzuni au hasira.
- Mzungumzaji anaweza kuuliza
maswali, kuona hisia za mzungumzaji kwa kusikiliza lugha zinazotolewa na
kuangalia ishara za mwili zinazotumika.
- Mzungumzaji anaweza kupata
nafasi ya kufuta usemi wake, kuongezea jambo au kutoa maelezo ya ziada.
Mzungumzaji anaweza kubadilisha lugha yake kulingana na mazingira aliyomo.
- Mzungumzaji anao uhuru wa
kutumia lugha ya mitaani, misimu kulingana na muktadha.
Matatizo ya lugha ya mazungumzo
- Maelezo lazima yahifadhiwe
kichwani, hivyo kama mtu hana kumbukumbu, taarifa zilizotolewa hupotea na
kusahaulika.
- Mtumiaji wa lugha ya mazungumzo
anaweza kurudiarudia vipengele fulani na hivyo kuichosha hadhira.
- Ujumbe unaweza usieleweka kama
unatolewa kwenye kelele nyingi
Lugha
ya maandishi
Hii ni lugha inayowasilishwa kwa
njia ya maandishi. Lugha ya maandishi huzihusiha pande mbili, mwandishi na
msomaji. Lugha ya maandishi sharti iwe fasaha ili msomaji anaposoma maandishi
hayo, apate kuelewa kila kitu, yaani asibaki akijiuliza maswali.
Lugha ya maandishi huambatana na
alama za uakifishaaji, hii husaidia maandishi kusomeka vizuri na kueleweka kwa
urahisi
Ubora wa lugha ya maandishi
- Lugha ya maandishi huwawezesha
watu walio mbali kuwasiliana.
- Lugha ya maandishi hustawisha
sarufi ya lugha na misingi yake, kwa sababu mwandishi anahakikisha kwamba
anazingatia vizuri kanuni za kisarufi ili msomaji wake aweze kumwelewa.
- Ili kuhakikisha maelezo yake
yanaeleweka mwandishi analazimika kuandika kwa uwazi na kwa kuzingatia
kanuni na miiko yote ya uandishi.
Udhaifu wa lugha ya maandishi
- Lugha hii hutumiwa na wale tu
wanaojua kusoma na kuandika.
- Lugha ya maandishi haina
msisimko uletwao na lafudhi na matamshi.
- Msomaji hukosa vidokezo vingi
ambavyo katika lugha ya mazungumzo huchangia katika mawasiliano.
- Lugha ya maandshi inamnyima
mwandishi nafasi ya kupima welewa wa msomaji kwa kuwa hamwoni.
Dhima
ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi
Lugha ya mazungumzo na lugha ya
maandshi zote zina umuhimu wa pekee katika maisha ya kila siku kwa sababu ndizo
zinzaowezesha watu kuwasiliana kwa namna mbalimbali.
Umuhimu wa lugha ya maandshi pia
hutokana na dhima yake kwa watu. Maandishi yanaweza kuhifadhiwa na kusambazwa
kwa watu wengi hata walio mbali. Maandishi yanahifadhi kumbukumbu na kwa muda
mrefu. Kwa hali hii, watu wa vizazi vingine wanaweza kusoma na kujua mambo
yaliyofanyika karne nyingi zilizopita.
Tofauti kati ya lugha ya mazungumzo
na lugha ya maandishi
- Lugha ya mazungumzo huwezesha
mawasiliano ya ana kwa ana lakini lugha ya maandishi haiwezeshi
mawasiliano ya ana kwa ana.
- Lugha ya mazungumzo haihitaji
maandalizi wakati lugha ya maandishi huhitaji maandalizi. Mwandishi
atalazimika kupata muda wa kuandika pamoja na kuandaa vifaa kama vile
kalamu, karatasi n.k
- Lugha ya mazungumzo hailazimiki
kuzingatia kanuni za kisarufi, lakini lugha ya maandshi hutakiwa
kuzingatia kanuni za kisarufi.
Tofauti nyingine kati ya lugha ya
maandishi na lugha ya mazungumzo huweza kuonyeshwa katika jedwali lifuatalo.
Kipengele |
Mazungumzo |
Maandishi |
Muktadha |
|
|
Mada |
Hazina
uzito mkubwa |
Huelekea
kuwa na uzito mkubwa. |
Mpangilio wa mada na mawazo |
Hautabiriki.
Unaelekea kutokuwa na mtiririko. |
Hutabirika.
Huelekea kuwa na mtiririko. |
Mjadala wa mada |
Hauelekei
kuwa na kina. Hazichujwi kwa uaangalifu. |
Unaelekea
kuwa na kina. Huchujwa. |
Dhima ya matumizi ya lugha
Dhima kuu ya lugha ni kupashana
habari, ujuzi na maarifa mbalimbali. Vilevile lugha husaidia kujenga uhusiano
mwema baina ya watu. Uhusiano huo unaweza kuwa wa kijamii, kielimu, kibiashara,
kihuduma, kisiasa, kiuchumi n.k. Kwa hiyo, kujua jinsi ya kuitumia lugha kama
inavyotakiwa, kunasaidia kufikisha vizuri ujumbe unaotakiwa bila kuupotosha.
Vilevile kunasaidia kuepuka migongano, hasa ya kijamii kwa kuwa utakuwa
umetumia lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii inayohusika.
Mambo ya kuzingatia katika matumizi
ya lugha
- Mada inayozungumziwa:Mada za mazungumzo zipo nyingi. Kuna mada za kijamii,
kwa mafano ndoa, unyago, mapenzi, kifo, matanga, burudani, muziki n.k.
Kuna mada za kibiashara kwa mfano bidhaa, kodi, vibali, fedha, hasara,
faida n.k. Kwa hiyo, ili mazungumzo yaweze kwenda vizuri, wazungumzaji
wanatakiwa kuzingatia mada husika.
- Muktadha wa mazungumzo:Mazungumzo yanaweza kuathiriwa na miktadha tofauti. Kwa mfano kuna miktadha ya kidini, kiganga, huzuni, sherehe, kisiasa, kielimu, kibiashara n.k. Mazungumzo yanaweza kufanyika mjini, kijijini, ugenini, shuleni, dukani, hotelini n.k
- Malengo ya mazungumzo hayo:Malengo ya mazungumzo nayo yanaathiri matumizi ya lugha. Kwa mfano, lengo linaweza kutoa taarifa, kuhoji, kukejeli, kutia moyo n.k. Sasa jinsi lugha itakavyotumika katika kutoa taarifa ni tofauti na itakavyotumika katika kutia moyo au kukejeli.
- Uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji:Matumizi ya lugha huweza kuathiriwa pia na mahusiano ya wazungumzaji. Kuna mazungumzo baina ya watoto, wanafunzi, wazee, viongozi, marafiki n.k. Upo uhusiano wa daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, mnunuzi na muuzaji. Kwa hiyo mazingira baina ya pande hizi mbili yatategemea uhusiano wao, kwa hiyo kaida za uhusiano huu utapaswa kuzingatiwa. Kwa hiyo, kwa kuzingatia mambo haya manne, itawafanya wazungumzaji wawe makini katika uteuzi wa maneno, miundo, mifano na kina cha ufafanuzi wa maelezo au habari inayozungumzwa.
Dhima
ya Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi
Lugha ya kimazungumzo na ya
kimaandishi zina dhima kuu ya kupasha habari, ujuzi, na maarifa mbalimbali,
husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu, kufikisha ujumbe unaotakiwa
vizuri bila kupotosha, kufundishia ujuzi, kuchochea maendeleo, kuhifadhi
historia ya jamii na kueleza mawazo au hisia za watu.
Lugha ya Kimazungumzo na ya
Kimaandishi katika Miktadha Sahihi
Tumia lugha ya kimazungumzo na ya
kimaandishi katika miktadha sahihi
Matumizi ya lugha ya kimazungumzo na
ya kimaandishi katika muktadha sahihi huongozwa na mambo yafuatayo, ambayo ni
mada inayozungumzwa, muktadha au mahali mazungumzo hayo yanapofanyika, malengo
ya mazungumzo hayo na uhusiano uliopo kati ya wazungumzaji.
Zoezi1.
Tumia lugha ya kimazungumzo na ya
kimaandishi katika miktadha sahihi.
Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili
Matamshi ni namna ambavyo mtu
anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha. Unaposema fulani ana matamshi
mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha anazungumza Kiswahili fasaha.
Neno moja linaweza
kuzungumzwa/kutamkwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali kutokana na sababu
mbali mbali, sababu hizo ni pamoja na eneo la kijiografia anakotoka huyo mtu,
kabila lake, kundi lake la kijamii mfano msanii au mwanasiasa, na elimu
aliyonayo. Hizi zote zinaweza zikawa ni sababu za kufanya watu watofautiane
katika matamshi.
Lafudhi Mbalimbali za Kiswahili
Dhana ya matamshi huhusisha
- Sauti za lugha husika
- Mkazo
- Kiimbo
Sauti za lugha ya Kiswahili
Sauti za lugha ya Kiswahili
hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla huunda sauti 24, irabu tano
na konsonanti 19 (konsonanti x na q hazipo katika matamshi ya kiswahili). Sauti
za Kiswahili hutamkwa kama zilivyoandikwa, kwa mfano maneno “data” au “dengue”
wewe unayatamkaje? Wengi huyatamka kama yalivyo hata kama wakiwa wanazungumza
kiingereza, hii ni kwa sababu maneno ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa.
Kwa hiyo unapotamka maneno ya
Kiswahili ni sharti uzingatie sauti asilia za lugha ya Kiswahili. Kuna watu
huwa wanaandika hivi “xaxa”, hii huwa unaitamkaje?Au “ucjal” huwa unaitamkaje?
Kwa kufuata matamshi asilia ya Kiswahili “ucjal” itatamkwa “uchijal” sijui
itakuwa ina maana gani sasa. Na pengine umekuwa ukitumia maandishi ya namna hii
hata kwenye insha zako ukidhani upo sahihi au ni kwa mazoea tu, sasa kwa kuwa
umejua matamshi sahihi ya Kiswahili ni yapi, utajifunza kuyatumia kwa usahihi
katika maandishi rasmi na yasiyo rasmi.
Mkazo
Katika lugha ya Kiswahili kuna namna
ya kutamka maneno ili kuleta maana mbali mbali, kwa mfano neno “barabara”
litaleta maana husika kulingana na jinsi lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni pale
silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo
hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa
mkazo, sauti hupandishwa juu kiasi.
Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale
yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho.
Kwa mfano:ba’bu, maya’i, rama’ni
(mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba'ra (njia).
Baadhi ya maneno yenye asili ya
kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine. Kwa mfano: bara'bara (sawa
sawa), Alha’misi
Kiimbo
Ni utaratibu maalum wa upandaji na
ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani.
Katika utaratibu wa utamkaji, dhana
ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu ( yaani , kiwango
cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj), Kwa hivyo ni muhimu
hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kiimbo kina
maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya
kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au
kuwa chini.
Aina za viimbo
- Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji
wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji
wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka. Mfano, Mwalimu
anafundisha.
- Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango
tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Mfano,
mwalimu anafundisha?
- Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiyani sana na kiimbo cha
maulizo. Kiimbo cha amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko
ilivyo katika kiimbo cha maelezo. Mfano, njoo hapa!
Lafudhi
ya Kiswahili
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa
lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo
yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu,
tabaka lake la kijamii na kadhalika.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili
kwa watumiaji wengi wa afrika mashariki, kwa hiyo hii inafanya kuwatambua
wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au maeneo wanakotoka.
Kwa mfano, kwa hapa Tanzania
tunaweza kuwatambua watu wa mwanza kwa lafudhi yao, watu wa mtwara kwa lafudhi
yao, watu wa pemba kwa lafudhi yao au watu wa Musoma kwa lafudhi yao.
Mfano 3.
- Usiniretee maswara ya ubaguzi
wa kikabira hapa (Wakuria)
- Amemupiga mutoto ya watu juu
amemuibia mfaranga makumi mawili (Wakongo)
- Ukikaa nchale, ukichimama
nchale (Wamakonde)
- Wewe unakamuaga mang’ombe tu
moja kwa moja (Wasukuma)
- Mbona unakuwa kinganganizi,
nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu! (Wahaya)
Utata katika Mawasiliano
Utata ni hali
ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo tungo tata ni tungo
ambayo inaweza kuwa na maana zaidi ya moja.
Sababu za Utata
Utata katika
tungo hutokea kwa sababu zifuatazo:
- Neno kuwa
na maana zaidi ya moja, kwa mfano neno mbuzi, kata n.k.
- Kutozingatia
taratibu za uandishi, Mfano; Tulimkuta Nyammy na rafiki yake, MazalavsTulimkuta
Nyammy na rafiki yake Mazala. Katika sentensi hizi alama (,) ndio
huleta tofauti, sentensi ya kwanza inamaana kulikuwa na watu wawili Nyammy
na rafiki yake aitwaye Mazala na sentensi ya pili isiyo na alama (,)
inamaanisha kulikuwa na watu wawili Nyammy na mtu mwingine ambaye ni
rafiki yake Mazala
- Kutumia
maneno bila kuzingatia muktadha wa matumizi ya maneno hayo.
- Utamkaji
wa maneno. Wakati mwingine utata unaweza kujitokeza katika matamshi tu,
ili hali katika maandishi utata hauonekani. Kwa mfano; Mimina wewe, katika
maandishi linaweza kuandikwa mimi na wewe, na hivyo kuondoa utata.
- Mjengo wa
maneno. Utata huu huzuka katika vitenzi kamapigia. Chanzo cha utata katika kitenzi hiki ni kiambishi –i-.
Kiambishi hiki kinaweza kumaanisha: kwa ajili ya…, kwa sababu ya.., kwa
kutumia chombo fulani.., au mahali fulani.
Mfano 4
Mfano:
- Alimpigia ukorofi wake (kwa
sababu ya)
- Alimpigia kiatu (kifaa)
- Alimpigia ndani (mahali)
Mfano 5
Mifano ya utata katika tungo
- Patience amemwandikia Lilian
barua:Sentensi hii huweza kuwa na
maana kuwa Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au Patience ameandika
barua kwa niaba ya Lilian
- Umefanikiwa kununua mbuzi?Sentensi hii huweza kumaanisha ununuzi wa mbuzi mnyama
au mbuzi kifaa cha kukunia nazi.
- Alimkuta amelala kwenye nyumba
ya wageni:Sentensi hii huweza kumaanisha,
nyumba ya mtu lakini inatumika kwa ajili ya wageni kwa malipo au ni nyumba
inayomilikiwa na watu ambao ni wageni katika eneo lile.
- Attu ametumwa na Aritamba:Sentensi hii inaweza kueleweka kumaanisha, Aritamba
amemtuma Attu au Attu na Aritamba wametumwa wote kwa pamoja
MADA YA TATU: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi kama zilivyo kazi
nyingine za fasihi andishi hufanyiwa uhakiki. Uhakiki huu huzingatia vipengele
vya fani na maudhui ili kubainisha usanaa wa kazi husika pamoja na kile ilichokusudia
kufikishwa kwa hadhira.
Uhakiki wa Ushairi
Mashairi kama kazi nyingine za
kifasihi huhakikiwa kwa kutumia vigezo sawa na vinavyotumika katika kazi
nyingine za kifasihi. Vigezo hivyo ni kwa kuzingatia vipengele vyake viwili
yaani fani na maudhui.
Vipengele
vya Fani na Maudhui katika Kuhakiki Ushairi
Elezea vipengele vya fani na maudhui
katika kuhakiki ushairi
Vipengele vya fani
Uhakiki wa fani za ushairi ni
uchambuzi wa kina na kuziweka wazi mbinu za kisanaa alizotumia mshairi katika kutunga
kazi yake. Vipengele muhimu vya kuhakiki katika fani ya ushairi ni kama
vifuatavyo:
Mtindo
Jambo la
kuonyesha hapa ni kwamba iwapo shairi ni la kimapokeo ama ni la kisasa.
Muundo
Katika kuhakiki
muundo wa shairi mhakiki inatakiwa aweke wazi mambo yafutayo:
- Idadi ya beti
- Idadi ya
mistari na aina ya vibwagizo
- Idadi ya vipande
- Idadi ya mizani
- Aina na mpangilio wa vina
Wahusika
Ikiwa shairi limehusisha wahusika ni
vema pia mhakiki awabainishe
Matumizi ya lugha
Katika kipengele hiki mhakiki huchunguza:
- Mpangilio wa maneno. Mf. Wengi
wari badala ya wari wengi
- Matumizi ya : Mazida –
kurefusha neno mfano, kiwembe badala ya wembe; Ikisari – kufupisha
neno mfano siombe badala ya usiombe; Tabdila – kubadilisha
mwendelezo wa neno mfano kujitanuwa badala ya kujitanua.
- Matumizi ya methali, misemo na
nahau
- Matumizi ya lugha ya picha
- Matumizi
ya tamathali za semi kama vile takriri, sitiari n.k
- Mbinu nyingine za kisanaa
Mhakiki anapochunguza vipengele vya
fani, jambo muhimu la kuzingatia ni jinsi vipengele hivyo vinavyosaidia
kuwasilisha maudhui.
Vipengele vya maudhui
Ili kuhakiki na kupata maudhui ya
shairi inatakiwa kulisoma shairi kwa kulielewa zaidi. Baada ya kupata picha
fulani kuhusu shairi na kutafakari maana za maneno muhimu, itatubidi tuelewe
vipengele vya maudhui, ambavyo ni dhamira, mtazamo, msimamo, falsafa ya
mwandishi, ujumbe na maadili, migogoro na muktadha.
Uhakiki wa Maigizo
Igizo huhakikiwa kwa namna lilivyo
katika maumbo yake yote mawili yaani fani na maudhui.
Vipengele vya Fani na Maudhui katika
Kuhakiki Maigizo
Elezea vipengele vya fani na maudhui
katika kuhakiki maigizo
Fani
Uhakiki wa fani katika maigizo
unajihusisha na ufundi uliotumiwa. Ufundi huu unajumuisha mambo kadhaa kama ifuatavyo:
Mtindo
Mtindo ni sura ya maigizo
inayojitokeza kupitia mpangilio wa maneno na vitendo. Inabidi mhakiki achunguze
kama kazi ni:
- Mchezo wa jukwaani – wenye
mpangilio wa mazungumzo baina ya watu na matendo yao.
- Majigambo
- Vichekesho – mpangilio wa
maneno yanayowasilisha ujumbe kwa kuchekesha.
- Mazungumzo – maongezi ya
kujibizana baina ya watu.
- Ngonjera – mpangilio wa tungo
za kishairi ambapo watu wawili au makundi mawili hukinzana.
- Miviga – sherehe za kitamaduni
kama vile matambiko
Pamoja na haya, mtindo hutegemea
lengo la maigizo ambalo laweza kuwa kuelimisha, kukejeli, kuburudisha, kuonya,
kukosoa na kadhalika.
Mandhari
Mazingira ya
kutendea ni kipengele muhimu cha fani. Mhakiki hana budi kujiuliza iwapo
utendaji unadhihirisha wakati au mahali halisi.Jambo hili huweza kutekelezwa
kupitia vifaa, maleba, maneno n.k.
Wahusika
Maswali ya
mhakiki kuuliza ni:
- Wamejitokeza kikamilifu?
- Wanaaminika?
Matumizi ya lugha
Vigezo anavyotumia mhakiki
kuchunguza lugha ni:
- Kama usemaji ni wa kisanaa,
yaani unatumia picha, tamathali za semi, methali, nahau n.k.
- Kama lugha imetumika vile
inavyotumiwa katika jamii. Mfano: kiimbo, mkazo, miguno, vihisishi n.k.
- Matumizi ya maneno ya ajabu
kama yale yanayotumiwa na waganga.
Maleba na vifaa
Hivi huakisi mandhari na husaidia
kuzua mukatadha. Kwa hiyo ni muhimu kuchunguza kama vimetumiwa ipasavyo.
Matumizi ya ala
Matumizi ya ala kama ngoma,
baragumu, au sauti zingine ili kuamsha hisia za hadhira ni jambo muhimu
kuchunguza.
Mbinu nyingine
Mhakiki anapaswa pia kuchunguza
matumizi ya nyimbo, uchezaji ngoma, usimulizi na mbinu nyingine katika kuibua
hisia za watazamaji.
Maudhui
Kwa upande wa maudhui, mhakiki wa
maudhui hutakiwa kuchunguza vipengele vyote vya kimaudhui ambavyo ni dhamira,
migogoro, maadili, mtazamo na msimamo wa fanani pamoja na ujumbe bila kusahau
kipengele cha falsafa. Yote hayo kwa pamoja ndiyo humsaidia mhakiki kubaini
ukinzani wa igizo na maisha halisi ya jamii ambayo huwa ndiyo hadhira ya igizo
hilo.
MADA YA NNE: UHIFADHI WA KAZI YA FASIHI SIMULIZI
Ili kitu kidumu ni lazima
kihifadhiwe; fasihi simulizi kama sanaa kutokana na umuhimu wake katika jamii
nayo huhifadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho. Katika mada hii utaweza
kujifunza umuhimu wa fasihi simulizi katika jamii. Utajifunza njia mbalimbali
zitumikazo katika uhifadhi wa fasihi simulizi pia utaweza kubainisha ubora na
udhaifu wa kila njia.
Njia za kuhifadhi Fasihi
Simulizi
·
Kuhifadhi Fasihi Simulizi
·
Bainisha njia za kuhifadhi fasihi
simulizi
·
Umuhimu wa kazi za fasihi simulizi
Ingawa kila utanzu wa fasihi una
umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zake zote zina umuhimu mkubwa katika jamii.
ü Kwaza fasihi hutumika kama chombo cha kuwaelimisha watu.
Kupitia fasihi andishi na fasihi simulizi, watu hupata maarifa ya kutambua
mambo maovu na namna ya kuyakwepa. Licha ya haya, wanajamii hujifunza njia za
kujitawala, kuzalisha mali na kuishi kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia.
ü Pili, fasihi ni nyenzo ya kutoa mafunzo kuhusu mambo kama
vile historia, dini, siasa, jiografia na tiba. Kwa hiyo watu hujifahamisha juu
ya maumbile na asili yake, mazingira, utawala, uchumi, sheria n.k.
ü Aidha fasihi huwapa watu mazoezi na kuimarisha uwezo wao wa
kuzungumza kwa ufasaha, kuimba nyimbo kwa ufundi, kuigiza mambo kwa ustadi,
kucheza ngoma kwa umahiri, kughani mashairi kwa mvuto na kusimulia matukio kwa
mtindo ufaao.
ü Fasihi hufahamisha, huhifadhi na hurithisha mambo kuhusu
utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mambo hayo ni pamoja na mila, desturi,
falsafa, imani na itikadi. Pia hudumisha maarifa ya kijadi kama vile tiba,
sayansi ya kilimo, uhifadhi wa mazingira na sayansi ya utabiri wa hali ya hewa.
ü Umuhimu mwingine wa fasihi unatokana na
kutumika kwake kama chombo cha kuburudisha na kupumbaza. Watu wanaposoma kazi
mbalimbali za fasihi hupata, msisimko wa kimwili na kiakili. Kadhalika fasihi
hugusa hisia za watu na kuwafanya wafurahi au wahuzunike.
ü Istoshe fasihi hudumisha na kukuza lugha. Watu hupanua
msamiati wao na miundo ya lugha kupitia kazi zake. Hivyo fasihi inakuwa kama
hazina ya maneno na dafina ya kanuni za kisarufi.
v Kutokana na umuhimu huu ndio maana fasihi huhifadhiwa ili
isipotee. Na uhifadhi huu hufanyika kwa njia mabalimbali.
Ubora
na Udhaifu wa kila Njia ya Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi
·
Elezea ubora na udhaifu wa kila njia
ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi
Fasihi simulizi inaweza kuhifadhiwa
kwa njia zifuatazo:
i.
Kichwani
Hii ndio njia ambayo imekuwa
ikitumiwa kuhifadhi kazi za fasihi tangu kale na inaendelea kutumika hadi leo.
Kwa kutumia njia hii kazi ya msanii hukaa kwenye ubongo wa msanii, naye huweza
kuiwasilisha kazi hiyo, wakati wowote bila gharama yoyote.
ü Ubora
wake
- Uwasilishaji wa kazi hiyo
unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji kufanyika maandalizi yoyote,
hususani ya kiufundi.
- Hakuna gharama yoyote wakati wa
uwasilishaji wa kazi ya fashi. Msanii hahitaji kugharimia kitu chochote
ili waweze kuitoa kichwani, ni uamzi wake tu, anaweza kuimba papo kwa
papo.
- Kazi ya fasihi iliyohifadhiwa
kichwani ni hai. Hii ni kwa sababu msanii anakuwa ana kwa ana na hadhira
yake. Kutokana na matumizi ya mbinu tofauti za kisanaa kama vile kucheza,
kubadili sauti, miondoko na mengineyo mengi, kazi yake inapata uhalisia
zaidi mbele ya hadhira.
ü Udhaifu
wake
- Uwezekano wa kazi kupotea au
kuharibika hasa katika fani ni mkubwa. Kwa mfano msanii anapokuwa
amefariki dunia kazi anayokuwa ameihifadhi kichwani nayo hupotea. Ndio
maana katika baadhi ya jamii kazi za kifasihi zimepotea. Hii ni kwa sababu
wasanii wanapoondoka duniani hondoka na fani hizo.
- Kazi inapohifadhiwa kichwani ni
rahisi kubadilika. Hii inatokea pale ambapo msanii anasahau baadhi ya
maneno kutokana na umri wake au sababu nyinginezo
ii.
Njia ya maandishi
Maandishi ni njia moja wapo
inayotumika kuhifadhia kazi za fasihi. Njia hii imeanza kutumika baada ya watu
kujua kusoma na kuandika. Uhifadhi wa kazi za fasihi kwa njia hii hupitia njia
mbili kubwa. Hatua ya kwanza ni kubuni kisa au wazo; na hatua ya pili ni
kuliweka wazo hilo katika maandishi. Kazi za fasihi simulizi zinazoweza
kuhifadhiwa katika maandishi ni hadithi, nyimbo, mashairi, ngonjera, majigambo
n.k
ü Ubora wake
- Kazi iliyohifadhiwa inaweza
kudumu kwa muda mrefu
- Kazi iliyohifadhiwa inaweza
kufikia hadhira hata ya mbali na aliko msanii.
- Kazi iliyohifadhiwa katika
maandshi haipotezi fani yake na maudhui yake bali huendelea kuwa katika
asili yake ya awali hadi msanii atakapoamua kuibadilisha.
ü Udhaifu
wake
- Hii njia ni kwa ajili ya watu
wachache tu wanaojua kusoma na kuandika.
- Wasanii wanaoweza kutumia njia
hii ni wale tu wanaojua kusoma na kuandika.
- Ni aghali sana kuhifadhi kazi
za kifasihi kwa njia ya maandishi. Msanii atalazimika kununua vifaa
vinavyohitajika katika maandishi ambavyo ni kalamu, karatasi, meza. Kwa
hiyo ni aghali.
- Uwasilishaji wake si hai kwani
hakuna kuonana ana kwa ana kati ya hadhira na fanani. Kwa hiyo msomaji
hawezi pata vionjo vya msanii hivyo itambidi ajibunie yeye mwenyewe.
- Wahusika pia hawawezi
kuonekana, endapo ni igizo mabalo limehifadhiwa katika maandishi, hivyo
ubora wa kazi ya msanii huchujuka.
iii.
Njia ya vinasasauti
Vinasasauti ni miongoni mwa vyombo
vinavyotumika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi. Hii ni njia iliyoendelea
kuliko ile ya maandishi.
ü Ubora wake
- Kazi ya msanii huweza kuwafikia
watu hata walio mbali na alipo mtunzi.
- Ikihifadhiwa katika vinasasauti
kama vile tepurekoda au CD ubora wake huwa haupotei wala kuharibika endapo
vifaa hivyo vitatunzwa vizuri.
- Sauti ya
mtunzi unaiskia moja kwa moja
- Unaweza kusikia vionjo vya
msanii
ü Udhaifu wake
- Njia hii
ni aghali kutumia, kununua vinasasauti ni gharama.
- Uwasilishaji
wake si hai, ingawa unaweza sikia sauti ya msanii au wahusika lakini
hahawezi kuonekana.
- Kazi
yoyote ya kifasihi inapohifadhiwa katika vinasasauti, kwa mfano nyimbo,
huwa ni mali ya msanii husika, mtu yeyote haruhusiwi kuitumia kama mali
yake binafsi bila kuruhusiwa na msanii.
iv.
Njia ya kompyuta
Njia hii imeanza kutumika katika
miaka ya hivi karibuni baada ya watu kuanza kujua na mna ya kutumia kompyuta.
ü Ubora wake
- Njia hii ni ya uhakika zaidi
kwa vile shuguli za kisanaa zinazohusika huhifadhiwa katika kompyuta na
hutolewa pale zinapokuwa zinahitajika.
ü Udhaifu
- Msanii au wasanii wanohusika
hawawasiliani na hadhira papo kwa papo. Hivyo hadhira hukosa kuuliza
maswali katika vipengele vinavyotatiza.
- Ili kuhifadhi kazi ya fasihi
kwa kutumia njia hii ni sharti msanii awe anajua kutumia kompyuta.
- Pia ni aghali sana, kuzingatia
kwamba kununua komputa ni gharama kubwa.
v.
Njia ya kanda za video
Msanii huweza kutumia kanda ya video
kuhifadhi kazi yake.
Ubora
wake
- Kwanza wasnii na vifaa
wanavyotumia huonekana
- Sauti zao na milio ya ala
wanazotumia husikika na pia huonekana kwa hadhira. Hii angalau huipa uhai
kazi ya msanii mbele ya hadhira.
- Huweza kudumu kwa muda mrefu
endapo kanda ya video iliyotumika kuhifadhi kazi ya msanii itatunzwa
vizuri.
Udhaifu
wake
- Uhifadhi wa njia hii ni aghali,
msanii atahitajika kununua, kanda ya video, kumlipa mpiga picha na
mzalishaji pia.
- Watu wanoweza kunufaika na njia
hii ni wacheche mno na wengi wao ni wale wenye uwezo wa kumiliki
televisheni ambao kimsingi hupatikana maeneo ya mijini.
- Ingawaje hadhira wanaweza
kumwona msanii lakini hawawezi kuwasiliana nae ana kwa ana, hivyo kukosa
kuuliza swali pindi wanapohitaji kufanya hivyo.
Umuhimu wa kuhifadhi kazi
za Fasihi Simulizi
·
Faida
ya Kuhifadhi Fasihi Simulizi
·
Elezea faida ya kuhifadhi fasihi simulizi
Njia zote za
uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi zina umuhimu mkubwa katika ukuzaji na
uendelezaji wa utamaduni katika jamii. Kama ambavyo tumekwishaona, kazi za fasihi
simulizi huelimisha, huburudisha, hurithisha maarifa, maadili, pia ni vielelezo
vya utamaduni wetu wa asiili. Kwa ajili hiyo ni muhimu kuzihifadhi kazi hizo
zisiharibike wala kupotea ili ziendelee kutumika kutoka kizazi kimoja hadi
kingine.
Ni muhimu
ziendelee kuwepo ili kuhifadhi utamaduni wetu na huku vikitumika kama vivutio
vya watalii.
Kazi za fasihi
simulizi kwa upande mwingine ni sehemu ya ajira. Kwa mfano, shughuli
mabalimbali za kisanaa kama vile ngoma, maigizo na utunzi wa vitabu, vinawapatia
vipato baadhi ya wasanii. Hivyo ni muhimu zihifadhiwe.
Kazi za fasihi
simulizi pia ni kichocheo cha umoja na maelewano miongoni mwa jamii. Yote hayo
kwa ujumla wake yanabainisha kuwepo na haja ya kuendelea kuzikusanya,
kuzifanyia kazi, kuziendeleza, na kuzihifadhi kazi za fasihi simulizi.
MADA YA TANO:
UTUNGAJI WA KAZI ZA KIFASIHI
Kazi za fasihi
simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga kazi fulani
ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni mbalimbli
zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa ya
kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile
ngonjera, methali , nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza pia kanuni
zinazoongoza utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.
Mashairi
Kanuni za Utungaji wa Mashairi
Fafanua kanuni za utungaji wa
mashairi
Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi
atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo
ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja.
- Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake
ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
- Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni
harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka
kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?
- Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je,
unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako
unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?
- Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni
chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?
- Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni
sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki – je,
iko chini au juu (kelele)?
Uzoefu wa
Mwandishi
Uzoefu ni hali
ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi ana
uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo gani
ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana nayo
katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) kuna baadhi ya
watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana nailoni na je kama
yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?
Uchunguzi/utafiti
Uchunguzi
unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa.
Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi
zake.
Uchunguzi ili
ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje, anakulaje, analalaje,
anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na wenzane na mazingira
yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi kufanya utafiti wa kina
ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na akiwasilishaje ili aweze
kuikamata hadhira yake.
Mwandishi baada
ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi yake. Hapa sisi
tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika hatua ya
utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya hapo tutakuwa
tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo yatatuwezesha kutunga
mashairi.
Dhana ya shairi
Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa
kwa utaratibu katika mistari.Sauti za silabi hufanana
zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta
ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.
Mpango wa
maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na
burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi
ijapokuwa hazikuandikwa.
Mashairi yana
umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika mistari.
Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo kadhaa yanayotakiwa
kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:
- Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani
sawa.
- Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye
sauti ileile mwishoni mwa sentensi.
- Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari,
ubeti hadi ubeti.
- Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti.
Kuna vituo vya aina tatu:
·
Kituo cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi
mwisho bila kubadilika katika kila ubeti;
·
Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho
maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti;
·
Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho ambao maneno
yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.
Katika mashairi
(ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na maana
kamili.
Vipengele vya fani katika mashairi
Vipengele vya
fani katika shairi ni pamoja na:
- Jina / anwani
- Mandhari
- Wahusika
- Muundo –tathnia, tathlitha,
tarbia, tathamisa, sabilia n.k
- Mtindo – pindu, msisitizo, beti
kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni
chanzo cha ubeti unaofuatia.
Vipengele vya Maudhui kati mashairi
Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo, mtazamo, na dhamira za mwandishi
- Matumizi ya ushairi ni pamoja
na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza, kufundisha, kuburudisha, kukosoa,
na kadharika.
Baada ya hapa sasa unaweza kuanza
kutunga shairi lako la kwanza.
Kuigiza
Ngonjera
Igiza
ngonjera
Katika kuigiza ngonjera muigizaji
hana budi kuzingatia fani yenye kanuni zifuatazo; mtindo wa mashairi ya
kimapokeo, muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani, vina, vipande,
mishororo na beti, kuteua mandhari kutegemeana na mada, kuwepo kwa wahusika
wawili au zaidi au makundi mawili au zaidi na matumizi ya lugha ya kishairi.
Maigizo
·
Kanuni za Utungaji wa Maigizo
·
Elezea kanuni za utungaji wa maigizo
Maigizo ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya
watu au viumbe wengine yaani kuiga jinsi walivyoumbwa, wanavyotembea,
wanavyovaa, wanavyosema n.k
Kanuni na hatua za kutunga maigizo
- Kuchagua wazo, tendo, visa au
tukio la kuigizwa:Ni
lazima jambo hilo liwe na uzito, umuhimu au athari fulani katika jamii.
Matukio hubainika kutokana na utafiti. Matukio yanayoweza kuwa kiini cha
kutungiwa maigizo ni kama vile matumizi mabaya ya simu za mkononi, mitindo
ya mavazi, madhara ya uganga wa kienyeji, madhara ya UKIMWI n.k.
- Kuchagua muktadha au mahali pa
kutendeka kwa jambo:Muktadha
waweza kuwa ofisini, shuleni, kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala
n.k
- Kuamua mtindo wa kuwasilisha
jambo la kuigizwa:Hapa
mtunzi anaweza kutumia fumbo, vichekesho, historia, tanzia n.k.
Inashauriwa mtunzi kuchanganya mbinu ili kuongeza mvuto.
- Kupanga hoja kuu zinazojenga
maudhui ya igizo:Maudhui
hujikita katika migogoro au mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana
pale migogoro inapofikia kilele. Kwa mfano jamabazi sugu anapokamatwa.
- Kuweka mpangilio wa maonyesho:Maonyesho hujumuisha vitendo na hoja zinazokamilisha
sehemu inayobeba aina moja au zaidi ya maudhui. Sehemu kadhaa nazo hukaa
zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo mojawapo muhimu. Katika migawanyo
hii yapasa mtunzi atunge kauli na vitendo vinavyoandamana navyo.
- Kubuni wahusika na kuweka aina
au idadi yao kulingana na matukio:Mtunzi
anashauriwa kutumia wahusika wanaohitilafiana. Kwa mfano wazee, vijana,
wanawake, wanaume, wanene, wafupi n.k. Mtunzi akishawateua anaweza
kuwatungia kauli na zamu za matendo katika sehemu mbalimbali.
- Ni muhimu pia kwa mtunzi
kuwaumba wahusika wake na kuamua maleba yao:Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa kuzingatia mazingira. Kwa
mfano siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa ngozi, kutumia mkongojo na
kuvuta mtemba.
- Urefu wa
maigizo ni suala la kuamliwa kutegemea tukio
- Kutunga
maelezo kuhusu mandhari:Maumbile ya wahusika na vitendo vyao, ni muhimu
kuelezwa katika mabano.
- Kuandika
maigizo na kuhariri:Ni muhimu kutumia lugha ya kimazungumzo inayovutia,
yenye kuleta taharuki na yenye utamu unaoeleza maadili kwa mnato.
MADA YA SITA: UANDISHI
Insha za Hoja
Insha za hoja
ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea
msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia.
Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake.
Katika uandishi
wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo
analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo.
Ili hoja zote
zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi
kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na
ana msimamo gani kuhusu mada hiyo.
Muundo wa Insha
za Hoja
Elezea muundo
wa insha za hoja
Katika uandishi
wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:
- Kichwa cha
insha; kichwa
cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako. Kwa mfano:
Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
- Utangulizi; Mambo
yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na
kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha
yako.
- Kiini cha
insha;katika
kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha
yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja
ulizonazo katika mjadala wako.
Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha
Barua Rasmi
·
Dhima ya Barua Rasmi
·
Elezea dhima ya barua rasmi
Barua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za
barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa
mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka
kumbukumbu au marejeo.
Muundo wa Barua Rasmi
·
Elezea muundo wa barua rasmi
Barua rasmi au
barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa kawaida huwa na sehemu zifuatazo:
- Anwani ya mwaandishi -huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa
karatasi.
- Tarehe ya barua hiyo- tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
- Anuwani ya mpokeaji- Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto
wa karatasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.
- Salamu- Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa
kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa
barua rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina
lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui
mpokeaji wa barua, tumia bw/bi
- Mada- Kichwa
cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama
vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe
mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua
kiukamilifu.
- Utangulizi– Hukaa
chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja
ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.
- Ujumbe- Ujumbe
wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.
- Tamati–
mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu,
[jina], Sahihi
Simu
·
Dhima ya Simu ya Maandishi
·
Elezea dhima ya simu ya maandishi
Simu za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo
husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za kawaida.
Simu hizo
huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na shirika la posta. Simu za
maandishi hujulikana kama telegram.
Kwa kawaida
simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi
ni njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako
ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu.
Gharama za simu
za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe
unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa.
mfano 1
Mfano wa simu ya maandishi:
MUSA KINGAMBE SLP 5299 DSM
NJOO HARAKADADA MGONJWA LINGIDO
·
Kuandika Simu za Maandishi kwa
Kuzingatia Muundo na Taratibu za Uandishi
·
Andika simu za maandishi kwa
kuzingatia muundo na taratibu za uandishi
·
Muundo wa kuandika simu za maandishi
una mambo yafuatayo ya kuzingatia ambayo ni anwani ya mpelekewa taarifa, ujumbe
na jina la mwandishi au mtuma simu. Mambo mengine ya kuzingatia ni kuandika
maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya
maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa na posta.
Kazi
1
Andika simu za maandishi kwa
kuzingatia muundo na taratibu za uandishi
Kadi za Mialiko
Kadi
za mialiko ni aina ya karatasi ngumu
zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba mtu ahudhurie katika sherehe fulani kama
vile harusi, ubatizo mahafali n.k
·
Muundo wa Kadi ya Mialiko
·
Fafanua muundo wa kadi ya mialiko
Mambo
muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:
- Jina la mwandishi au mwalikaji
- Jina la
mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi., Bw. Bw&Bi n.k
- Lengo la mwaliko
- Mahali pa kufanyika shughuli
- Tarehe ya mwaliko
- Wakati wa shughuli
- Jina na anwani ya mtu
atakayepelekewa majibu.
Mialiko huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa katika kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile Bwana….Bi…..au Ndugu…ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na Bibi.
Mfano. 2
Mfano
wa Kadi ya Mwaliko
Familia ya Manyama na Joseph
Wanapenda kukualika/kuwaalika
Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye harusi ya kijana wao mpendwa
Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi wa simba siku ya
Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usiku
Kufika kwako ndio mafanikio ya
sherehe hii.
Majibu kwa
(wasiofika tu)
Emmanuel Joseph
Simu: 0786 67 54 62
Uandishi wa Dayolojia
v Dhana ya Dayolojia
v Elezea dhana ya dayolojia
Dayolojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi
wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utunagaji,
dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa nijia ya mazungumzo au maandishi.
Katika kutunga dayalojia mtunzi hana
budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari
kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo
kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu
kulingana na matendo yao.Kwa mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa,
vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali
ya mkulima halisi.
Mambo
ya kuzingatia katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:
- Kutoa maelezo ya ufafanuzi
katika mabano ili kumfahamisha
- Kuwa na mazungumzo ya mkato na
yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo
kupita wengine.
- Kutumia vihisishi ili kufanya
dayalojia iwe ya kusisimua
- Pawepo mwingiliano wa
mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.
Mfano wa 3
Mfano wa dayalojia
Wambura: |
(Anaonekana mwenye furaha,anamwita
rafiki yake, Anna)Wow, Anna! Tumekutana tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana
wote wakiwa na nyuso za furaha). |
Anna: |
(Anatabasamu huku ameshikilia
mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu)Wambura! Bado unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni
muda mrefu sana. |
Wambura: |
(Anachekelea)Aaaah, nahisi kama naota Neema, siamini kama nimekutana na
wee leo hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa kweli. |
Anna: |
(Anachekelea) |
Wambura: |
Mbona wachekelea tu…. |
MADA YA SABA:
USIMULIAJI WA MATUKIO
v Usimuliaji wa Matukio
v Njia za Usimulizi wa Matukio
v Fafanua njia za usimulizi wa matukio
Usimulizi hufanyika kwa njia kuu
mbili:
·
kwa njia ya maandishi
·
na kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
Kila njia hutegemea kwa namna
msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na
msikilizaji hawakukaribiana, njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi.
Kwa mfano kama utahitaji kumweleza
mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi,
yaani utatumia njia ya kumwandikia barua.
Lakini kama unamsimulia mtu ambaye
yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.
Taratibu
za usimulizi wa matukio
Usimulizi wa matukio dhamira yake ni
kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi
msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo muhimu ambayo yatawawezesha watu hao
kulielewa tukio linalosimuliwa sawasawa na huyo anayeshuhudia.
Mambo muhimu ya kutaja katika
usimulizi wa matukio ni pamoja na haya yafuatayo:
- Aina ya tukio – msimuliaji atatakiwa kubainisha katika maelezo yake
aina ya tukio. Kwa mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya
barabarani au mkutano.
- Mahali pa
tukio – ili
msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni lazima kumwelewesha ni
mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjini inafaa kutaja
hata jina la mtaa.
- Wakati – katika
usimulizi ni muhimu pia kutaja muda ambao tukio limetendeka kama ni
asubuhi, mchana au jioni bila kusahau kutaja muda halisi yaani ilikuwa saa
ngapi.
- Wahusika
wa tukio – ni muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani,
wingi wao, jinsia yao, umri wao n.k.
- Chanzo cha
tukio – kila
tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika usimulizi.
- Athari za
tukio – athari
za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali, je watu wangapi
wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.
- Hatima ya
tukio –
msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe baada ya tukio
kutokea na kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa mfano, kama tukio ni
ajali ya barabarani hatima yake inaweza kuwa majeruhi kupelekwa
hospitalini na dereva aliyehusika kukamatwa.
Kwa hiyo
misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na sehemu kuu tatu:
- Utangulizi – sehemu
hii huwa na maelezo tu ya utangulizi ambayo hulenga kuvuta hisia na
umakini wa msikilizaji au wasikilizaji. Kwa kawaida utangulizi wa tukio
huwa ni maneno machache kiasi yasiyozodi aya moja.
- Kiini – kiini
cha usimulizi huelezea tukio halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, muda,
mahali na athari za tukio.
- Mwisho – mwisho
wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio
linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maelezo
ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo
amesimulia.
Mbinu za usimulizi
Ili habari
inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za kusimulia
katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake.
Baadhi ya mbinu
hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi ya
Kiswahili.
Kwa upande wa
uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio ambalo
anasimulia. Nayo ni kama vile milio, sauti na matendo.
Kwa upande wa
usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti usimulizi huo uwe na
kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyozidi
matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.
Kwa vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika wakati uliopita.
MADA YA NANE: UFAHAMU
Ufahamu ni dhana
inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa
usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa
katika kusikiliza jambo au katika kusoma.
Ufahamu wa Kusikiliza
Ufahamu wa
kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa
mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna
fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza
humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena
kwa maneno yake mwenyewe.
Kujibu Maswali
ya Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza
Jibu maswali ya
ufahamu kutokana na habari uliyoisikiliza
Ufahamu wa
kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile
kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
- Kuelewa vizuri sarufi ya lugha
ile inayozungumzwa
- Kuelewa vyema maana ya maneno
ya mhusiaka anayezungumza
- Kuelewa sintaksia (muundo wa
maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza,
msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
- Kuwa makini na kuelekeza akili
yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
- Kutilia maanani vidokezo vya
maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha,
anafafanua au anahitimisha hoja.
- Msomaji anatakiwa kuandika
baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo
baadae.
- Kuwa makini na ishara mbambali
za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au
hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata
maana katika mazungumzo.
Kufupisha kwa Mdomo Habari
uliyoisikiliza
Fupisha kwa mdomo habari
uliyoisikiliza
Ili kuweza kufupisha kwa mdomo
habari uliyoisikiliza yapo mambo ya kuzingatia. Mambo hayo ni kubaini mawazo
makuu yanayopaswa yajitokeze katika habari iliyofupishwa, kupanga maelezo kwa
usahihi katika usemaji, kuzingatia kichwa cha habari ambacho kinapaswa
kihusiane na ufupisho na wazo kuu na mwisho ni kusema ufupisho kwa ufasaha na
kwa lugha ambayo ni nzuri.
Activity 1
Fupisha kwa mdomo habari uliyoisikiliza
Ufahamu wa Kusoma
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu
anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti.
Kusoma kwa Sauti kwa kuzingatia
Lafudhi ya Kiswahili
Soma kwa sauti kwa kuzingatia
lafudhi ya kiswahili
Kuna vipengele viwili vinavyounda
mchakato wa ufahamu wa kusoma:
- Uelewa wa msamiati na
- Uelewa wa matini
Ili kuilelewa habari/matini ni
lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo.
Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote hataeleweka.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji
anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa
ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa
analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake
basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
- Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya
hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia
alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
- Kubaini maana ya maneno na
misemo mbalimbali;
habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini
maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia
kuelewa vyema maana ya mwandishi.
- Vilevile msomaji anatakiwa
kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa
akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji
atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha
habari hiyo aliyoisoma.
Kujibu Maswali kutokana na Habari
uliyoisoma
Ili kujibu maswali yanayotokana na
habari uliyoisoma inatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo; kubaini mawazo makuu,
kuzingatia alama za uandishi, kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali na
kutilia maanani vidokezo vya maana.
Aidha mawazo yanapaswa kuelekezwa
katika jambo linalosomwa, kujiuliza maswali kadri unavyosoma na kuandika
ufupisho.
Kufupisha
Habari uliyoisoma
Ili kuandika ufupisho mzuri wa
habari uliyosoma yapaswa kuzingatia yafuatayo: kuisoma habari uliyopewa zaidi
ya mara moja, kubainisha mawazo makuu, kuandika ufupisho kwa lugha fasaha na
yenye mtirirko mzuri wa hoja, kuhesabu idadi ya maneno na kuhakikisha haizidi
idadi inayotakiwa na kupitia habari ya mwanzo na kisha ufupisho ili kuona kama
taarifa muhimu haijaachwa au kusahaulika
Kusoma kwa Burudani
Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu
huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi
magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.
Wakati mwingine sio lazima msomaji
awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida.
Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.
Ingawa lengo la msomaji huwa ni
kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti,
majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo mabalimbali
yanayoihusu jamii.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu
wa Kusikiliza
Mambo ya kuzingatia katika usomaji
kwa burudani
Msomaji kutokana na kusoma vitabu na
majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya
kijamaii yanayojadiliwa humo.
Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea
tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika
kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu w kuweka
kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.
Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima
na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani ni kama ufuatao:
- Tarehe...
- Jina la
kitabu/makala/gazeti....
- Mchapishaji......
- Mwaka/tarehe ya
uchapishaji.....
- Ufupisho
wa habari(yasizidi maneno 20)
- Fundisho/ujumbe mkuu ni.....
- Jambo lililokuvutia sana......
- Maoni kwa ujumla kama yapo....
Matumizi ya Kamusi
Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye
msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa
katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza
kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala tepe
yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na
kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa
kielekroniki.
Jinsi ya Kutumia Kamusi
Elezea jinsi ya kutumia kamusi
Maneno yanayoingizwa katika kamusi
hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza na herufia, yote
huwekwa chini ya herufiA. Maneno yanayoanza na herufi fulani nayo
hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya pili, ya tatu,
nne au tano ya neno kama mfano hapa chini unavyoonyesha.
Mfano:ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno yote
yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya tatu
ni [b] na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti maneno
yenye [b] kabla ya yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni mawili
itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa
mwanzo. Neno ‘jabali’ litaorodhewshwa kabla ya ‘jabiri’ kwa kuwa [a] (herufi ya
nne) ya ‘jabali’ hutangulia [i] ya ‘jabiri’ ambayo pia ni herufi ya nne. Kisha
tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya
nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya ‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa
kuwa [h] hutangulia [i] basi ‘jadhibika’ huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na
‘jadi’.
Kwa hiyo hivi
ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi ya neno
ulalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya kwanza
kuorodheshwa.
Neno
linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwakidahizo.Kidahizo
huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana
ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo
n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwa kitomeo cha kamusi.
Kutafuta maana
unayoitaka
Neno linaweza
kuwa na maana moja au zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji kamusi hana
tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno linapokuwa na
maana zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi aichague. Ili
kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana ambayo
inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.
Example 1
Mfano:kifungo nm vi-
- kitu cha kufungia
- kitu kinachotumiwa kufungia
vazi kama vile shati, gauni, suruali n.k
- adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa
muda fulani
Iwapo mtumiaji aliona neno ‘kifungo’
kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana
na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha huu itakuwa ni ile maana ya 3 kwa
sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo neno kifungo limetumika na wala
sio maana ya 1 wala ya 2.