Nafasi za Kujiunga Vyuo vya Ualimu Awali na Msingi 2025
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NA KUPOKEA MAJIBU
Utaratibu wa kutuma maombi na kupokea majibu utakuwa kama ifuatavyo:
(i) Wahitimu wa kidato cha nne, Kidato cha sita na Walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobainishwa katika tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi;
(ii) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielectroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://tcm.moe.go.tz/);
(iii) Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
(iv) Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
(v) Majibu kwa watakaogchaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia "Account" aliyoitumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 20/07/2025) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa;
(vi) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo visivyo vya Serikali watatuma maombi yao katika vyuo husika. Aidha, majibu kwa watakaogchaguliwa kujiunga na Mafunzo hayo yatatolewa na Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa;
(vii) Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangiwa mwombaji kwa kutumia anwani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa urahisi kwa mawasiliano zaidi.
(viii) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10/07/2025.