1.
Jina lako linafupi na utuambie
kidogo kuhusu wewe
Jibu: Ninaitwa
…, nina elimu ya …, na uzoefu wa kazi za usimamizi
wa nyaraka. Mimi ni makini, nina nidhamu na uwezo wa
kushughulikia kazi kwa wakati
2.
Kwa nini unataka nafasi ya Karani
Msaidizi katika uchaguzi?
Jibu: Nataka
kuchangia kuhakikisha uchaguzi
hufanyika kwa haki na nina ujuzi wa usimamizi wa nyaraka na data unaohitajika.
3.
Je, unafahamu majukumu ya Karani
Msaidizi katika uchaguzi?
Jibu: Kusimamia kuandikishwa kwa wapiga
kura, kukagua kadi za utambulisho, kuandaa nyaraka za
uchaguzi, na kuhakikisha taratibu zinafuatwa kwa usahihi.
4.
Una uzoefu wowote wa kazi zinazohusiana na usimamizi wa nyaraka, kuingiza data au utawala wa
ofisini?
Jibu: Ndiyo,
nimefanya kazi za kuandaa na kuhifadhi nyaraka,
kuingiza data kwenye
kompyuta na kupanga
kumbukumbu kwa usahihi.
5.
Je, umewahi kushughulikia
mabadiliko au msongo wa kazi?
Jibu: Ndio,
kwa kupanga vipaumbele, kusanifu ratiba na kushirikiana na wengine ili kuhakikisha
kazi inakamilika kwa wakati.
6. Ni hatua gani unazochukua kuhakikisha usahihi wa data na
nyaraka zako?
Jibu: Kupitia
mara mbili (double
check), kutumia checklist, na kuhakikisha nakala
za backup zinapatikana.
7.
Je, una ujuzi wa matumizi ya
kompyuta na programu za ofisi?
Jibu: Ndio,
ninaweza kutumia Word,
Excel na PDF, na nina uwezo wa kujifunza programu
mpya haraka.
8. Unaweza kufanya kazi kwa muda mrefu au usiku siku ya
uchaguzi?
Jibu: Ndio,
niko tayari kufanya
kazi muda wowote
inapohitajika kuhakikisha uchaguzi
unakamilika vizuri.
9.
Kwa nini tuchague wewe badala ya mtu mwingine?
Jibu: Mimi ni mwaminifu, nina nidhamu, nina ujuzi wa usimamizi wa nyaraka na nina uwezo
wa kufanya kazi bila usimamizi mkubwa.
10. Ni hali gani unaweza kukabiliana na migogoro au watu
wasiokubali matokeo ya uchaguzi?
Jibu: Nitakaa
mtulivu, kueleza taratibu
kwa upole, na ikiwa hali ni ngumu
nitaelekeza kwa msimamizi
mwenye mamlaka.