MWALIMU DARAJA LA III B - HISABATI (MATHEMATICS) - 150 POST
QUALIFICATIONS AND EXPERIENCE - MWALIMU III HISABATI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Nenda google andika portal.ajira.go.tz kisha search kuweza kuingia kwenye portal ya Sekretarieti ya Ajira. Utalogin au kutengeneza akaunti yako kama ni kwa mara ya kwanza. Nenda kwenye vacancies kisha search Mwalimu Daraja IIIB kisha soma details kuelewa Qualifications pamoja na Responsibilities. Andaa barua kisha tuma maombi kabla ya tarehe 26 mwezi huu wa sita.
Umuhimu wa Usaili 2025 Kupitia Ajira Portal
1. Kuthibitisha Ustahiki wa Waombaji Usaili ni njia ya kuhakiki kama mwombaji ana ujuzi, elimu, na uwezo unaohitajika kwa nafasi ya kazi. Kupitia usaili, waajiri wanaweza kutofautisha kati ya waombaji wenye sifa zinazofanana na kuchagua bora zaidi.
2. Kuhakikisha Uwiano wa Mahitaji ya Ajira na Rasilimali Watu Kwa kutumia Ajira Portal, serikali huweza kupanga usaili kwa kuzingatia mahitaji halisi ya sekta husika, kama afya, elimu, au utawala. Hii huwezesha upangaji bora wa rasilimali watu serikalini.
3. Kuhakikisha Uwiano na Uwazi katika Ajira Usaili kupitia Ajira Portal unatoa mazingira ya haki kwa waombaji wote. Mfumo huu hupunguza upendeleo, urasimu, na nafasi ya rushwa kwa kuwa kila hatua ya mchakato inafanyika kwa uwazi kupitia mfumo wa kidijitali.
4. Kuokoa Gharama na Muda Kwa kutumia mfumo wa Ajira Portal, sehemu kubwa ya mchakato wa usaili huanza mtandaoni kutuma maombi, kuchambua sifa, na hata kutuma wito wa usaili. Hii hupunguza muda na gharama kwa pande zote mbili serikali na waombaji.