Tangazo la Kuitwa Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania 2025

 

Tangazo la Kuitwa Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania 2025


Tangazo la Kuitwa Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania 2025

Kuitwa kwenye Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania - Tangazo la Kuitwa Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania 2025 June.

1. Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo. 

2. Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi. 

3. Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi. 

4. Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari. 

5. Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi ukiwa na simu ya mkononi. Yeyote atakayepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano. 

6. Kwa yeyote atakayeripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 14/06/2025 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo. 

7. Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo hili. 


DOWNLOAD PDF YA TANGAZO NA MAJINA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI

Next Post Previous Post