Download Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Pili (STNA) 2025 – NECTA - Necta Standard Two National Assessment Timetable 2025.
Kila mwaka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) huandaa mitihani mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Kwa wanafunzi wa darasa la pili, mtihani maalumu unaoitwa Standard Two National Assessment (STNA) huandaliwa ili kupima uelewa wa mwanafunzi katika masomo ya msingi. Ratiba ya mtihani huu ni nyaraka muhimu sana kwani ndiyo inayoonyesha ni lini na saa ngapi masomo husika yatafanyika.
Maana ya NECTA Standard Two Timetable 2025 (STNA)
Ratiba hii ni mwongozo rasmi wa mtihani wa darasa la pili mwaka 2025. Inawaonyesha walimu, wazazi na wanafunzi tarehe na muda wa kila somo. Kwa lugha rahisi, ratiba ni mpangilio wa siku na masaa ya mitihani, unaotolewa mapema ili kusaidia maandalizi.
Umuhimu wa Ratiba ya Mtihani Darasa la Pili STNA 2025
A. Inawasaidia wanafunzi kujiandaa kwa kila somo kwa wakati.
B. Wazazi na walezi hupata nafasi ya kupanga maandalizi ya vifaa na mahitaji ya watoto wao.
C. Shule hupata urahisi katika kupanga uangalizi na usimamizi wa mitihani.
D. Inapunguza hatari ya kuchanganyikiwa au kukosa mtihani.
Jinsi ya Kudownload Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Pili (STNA) 2025 – NECTA
1. Tembelea Website rasmi ya Necta Kupitia link hii necta.go.tz
2. Shuka kwenye uwanja wa Habari Mpya(News)
3. Utaona Batani ya STNA Timetable 2025, Gusa ili kufungua.
4. Baada ya kugusa batani ya STNA Timetable page nyingine ya Pdf ya Timetable itafunguka.
5. Bonyeza neno attachment kudownload Pdf ya Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Pili au Gusa batani nyekundu hapo chini kudownload Pdf ya STNA Timetable automatically.