Karibu Shuleforum, Kama ulikuwa unajiuliza ufanye nini ili uweze kufaulu Usaili wa Mazungumzo Kutoka Ajira ortal au Taasisi Mbalimbali za Umma basi makala hii imeandaliwa kwa Ajili yako.
Nini Maana ya Oral Interview?
Oral interview (Usaili wa Mazungumzo) ni aina ya usaili wa ana kwa ana ambapo mwombaji wa kazi (au nafasi fulani) huulizwa maswali mbele ya paneli ya waajiri au wachunguzi, na anajibu kwa mdomo, si kwa maandishi. Usaili huu wa Oral mara nyingi ni wa muda mfupi kati ya dakika 15 mpaka 30 itategemeana na majibu yako pamoja na taratibu za taasisi uliyoitwa kwenye usaili.
Utakapo Fika Usaili wa Oral au Kufaulu Usaili wa Written Kupitia Ajira Portal basi utakuwa na asilimia zaidi ya 85 kupata Ajira au Kuitwa Kazini Kupitia Sekretarieti ya Ajira Portal. Kama utapata Maksi 50 au Zaidi jina lako litahifadhiwa kwenye kanzidata kwa mwaka mmoja na itakapotokea nafasi ya kazi basi utaitwa kazini.
Ila Mara nyingi Maswali yanayoulizwa miongoni mwa hayo maswali yanatabirika haswa ya kujitambulisha wewe mwenyewe.
Je Usaili wa Oral Upoje?
Usaili wa Oral (Mazungumzo) Mara nyingi huwa na maswali saba au pungufu ya saba, lugha inayotumika zaidi ni Kiingereza ila kuna kada waliotumia lugha ya kiswahili wakati wa kujifunzia taaluma yao watatumia lugha ya kiswahili kwa kifupi lugha uliyokuwa unajifunzia chuo ndio lugha itakayotumika wakati wa usaili wa mazungumzo, Muda huwa kati ya dakika 15 mpaka 30 kwa Ajira Portal pia kutakuwa na Panel ambayo ndio watakao kuuliza maswali kwa kupokezana (Wanaweza kuwa 3 mpaka 7).
Nifanye Nini ili Niweze Kufaulu Usaili wa Oral 2025 Ajira Portal
Kwa Tafiti ndio iliyofanyika na wadau mbalimbali inaonesha kuwa wakati unajiandaa kwenda kwenye usaili wa mazungumzo lazima ujiandae na vitu hivi vifuatavyo:
1. Jambo la kwanza ni Kumtanguliza Mungu akupe utulivu wa nafsi na akili na kujiamini. Amini kuwa ndio wakati wako sasa wa kuonesha kile bora ulichonacho kupitia dhamana ambayo Mwenyezi Mungu amekupatia mpaka kufika hapo.
2. Jambo la Pili Jiandae kujibu swali la " TELL US ABOUT YOURSELF" swali hili limekuwa la lazima kwa kila kada huwa ndio swali la kwanza wanaloulizwa wote watakao shiriki usaili wa oral. Hakikisha unalijibu vizuri ili upate maksi nyingi ili iwe rahisi kwako kufikia maksi 50% au zaidi ili uweze kuitwa kazini. Hakikisha unajibu swali hili vizuri kwa kuzingatia engo zifuatazo:
- Jina lako/Majina yako
- Personal History yako
- Educational Background
- Your Experience
- Weakness and Your Strength + Hobbies.
