Necta Form Two Exam Timetable 2025/2026 ni nini?
Tunaposema Necta Form Two Exam Timetable au Form Two FTNA Exam Timetable hii ni ratiba ya mtihani wa upimaji kidato cha pili inayoonesha siku/tarehe ya kuanza mtihani wa upimaji wa taifa mpaka siku ya kumaliza kwa mpangilio wa masomo kwa kila siku ndani ya jumla ya siku zilizopangwa kufanyika mtihani huo.
FTNA inamaa ya Form Two National Assessment na Mitihani hii hufanyika kila mwaka mara moja na kuwapima wanafunzi wenye sifa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tatu. Wanafunzi wote watakaopata Matokeo mazuri au yale ya kuridhisha wataweza kuendelea na masomo ya kidato cha pili 2026 ila wale watakao kosa ufaulu wa mwisho uliowekwa na Baraza la Mitihani Necta watakosa sifa ya Kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tatu 2026.
Faida ya Kuwa na Necta Form Two Exam Timetable 2025/2026 Mapema?
1. Moja ya Faida kuwa baada ya kutangazwa kwa Ratiba ya Mitihani ya Upimaji kidato cha pili walimu pamoja na wanafunzi Akili zinachangamka na hapa ndipo linakuja lengo la final touch yaani wanafanya revision kubwa ya mwisho kuelekea mtihani wa Necta FTNA.
2. Inasaidia Walimu kupangilia vizuri muda wa revision/marudio ya mada/maswali mengi ndani ya muda na kufanikisha kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri Katika Mtihani wao wa Form Two National Assessment 2025.
3. Huwaandaa wanafunzi kisaikolojia kujua tarehe halisi ya mitihani kunawasaidia wanafunzi kujiandaa kiakili na kisaikolojia mapema.
4. Huwasaidia walimu kupanga majaribio ya mwisho (mock/revision) Walimu huweza kupanga majaribio au masomo ya marudio (revision classes) kwa ufanisi zaidi wakijua ratiba ya mtihani wa taifa.
5. Huwezesha shule kuandaa mazingira ya mtihani muda unapotangazwa mapema, shule huweza kupanga vyumba, wasimamizi na vifaa vinavyohitajika kwa wakati.
Jinsi ya Kudownload Form Two (FTNA) Exam Timetable 2025/2026
Ili uweze Kudownload Form Two (FTNA) Exam Timetable fuata hatua vifuatazo:
1. Nenda google andika necta.go.tz kisha search.
2. Kama itakuuliza uchague app kama chrome ili uweze kuendelea chagua kisha subiri website ya Necta ifunguke.
3. Baada ya page ya Necta kufunguka shuka chini kwenye sehemu ya Latest News za Necta utaona Ratiba ya mtihani wa Necta Kidato cha Pili 2025. Utagusa ili uweze Kudownload hapohapo.
Click Here to Download FTNA Exam Timetable 2025

