Waombaji Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Vyuo vya Veta Kwa Ngazi Ya Tatu 2025.
Fursa Mpya kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya Stadi VETA – Kazi ya Tatu, 2025
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeendelea kutoa nafasi muhimu kwa vijana wa Kitanzania kupitia Mafunzo ya Stadi za Kazi kwa ngazi ya tatu. Katika awamu hii mpya ya uchaguzi wa wanafunzi, orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo imetangazwa rasmi kwa mwaka wa masomo 2025.
Lengo la Mafunzo
Mafunzo haya yanakusudia kuwajengea vijana ujuzi wa vitendo katika sekta mbalimbali kama vile:
i. Ufundi wa umeme
ii. Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT)
iii. Useremala
iv. Uashi
v. Ushonaji
vi. Ufundi magari
vii. Huduma za hoteli na utalii