WhatsApp Group Join Now

Ads Area

Nafasi za Kazi Watendaji Vituo Vya Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025 Zanzibar

 

Nafasi za Kazi Watendaji Vituo Vya Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025 Zanzibar

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA TANZANIA ZANZIBAR

Kwa madhumuni ya uendeshaji wa uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kiki soma pamoja na kanuni ya 10(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo:

1. Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura

2. Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura

3. Makarani Waongoza Wapiga Kura

NAMNA YA KUTUMA BARUA YA MAOMBI

1. BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE ANUANI IFUATAYO:

Mkurugenzi wa Uchaguzi,

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,

Ofisi ya Zanzibar,

Mtaa wa Maisara,

S. L. P. 4670,

ZANZIBAR.


MUHIMU: Maombi yote yawasilishwe katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya husika kwa Unguja na Pemba. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa hayatafanyiwa kazi.

2. BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE NYUMA YA BAHASHA NAFASI ANAYOOMBWA MWOMBAJI AKITAJA WILAYA AU JIMBO ANALOTAKA KUFANYIA KAZI NA AAMBATISHE VYETI VYA ELIMU PAMOJA NA MAELEZO YA TAARIFA BINAFSI (CV).

MWOMBAJI ATAKAYEBAINIKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KUGHUSHI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 16 AGOSTI, 2025 SAA 9:30 ALASIRI

Limetolewa leo tarehe 03 Agosti, 2025 na:

(sahihi)

Kallima, R.K

MKURUGENZI WA UCHAGUZI 


DOWNLOAD PDF HERE 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad